Mikopo

Mkopo wa Biashara

Ni mkopo ambao unatolewa kwa watendakazi ambao tayari wanafanya Biashara. Aina hii ya mkopo Dhamana yake kubwa ni biashara yenyewe. Lazima mkopeshwaji awe na TIN pamoja na Lesseni ya Biashara. Pia vitu vingine ni pamoja na risiti ya malipo ya kodi (TAX CLEARANCE CERTIFICATE) na TAX Payment Slip. RIBA ya mkopo ni asilimia 1.67 kwa kila mwezi. Kiwango wa cha mkopo kinategemea na Akiba ya mwanachama.

Mkopo wa kilimo & Ufugaji

Mkopo wa namna hii hutolewa kwa mwanachama ambaye tayari anafanya shughuli za kilimo na ufungaji. mkopeshwaji atafanyiwa tathimini ya Team Leader kutoka klasta yake kisha kutuma majibu shalom saccos Limited. Riba ni asilimia 1.67, Kiwango cha mkopo kinategemea na uwezo wa shughuli Husika ya mkopeshwaji.

Mkopo wa Ujenzi/Nyumba

Mkopo wa Ujenzi au Nyumba ni Mkopo wa muda mrefu, mkopo huu unatolewa kuanzia miaka miwili hadi miaka mitano kwa Riba ya kiwango cha 20% kwa mwaka. Dhamana ya mkopo huu ni nyumba yenyewe. Mtendakazi anayekopa fedha kwa ajili ya Ujenzi wa nyumba atahitajika kuwa na hati ya kiwanja au barua/Mkataba wa mauziano ya kiwanja hicho na mmiliki. Endapo hana atahitajika kuwa na mkataba wa ajira ambao muda wake wa kuisha ni ndani ya muda wa mkopo huo.

Mkopo wa Kiwanja

Mkopo huu unatolewa kwa mtendakazi anayetaka kununua kiwanga eneo lolote lile. fedha za mkopo wa aina hii hulipwa moja kwa moja kwenye kampuni Husika; saccos itashughulikia hati miliki ya kiwanja na kumkabidhi mkopeshwaji siku ya kumaliza marejesho ya mkopo huo.

Mkopo wa Elimu

Mkopo wa elimu unatolewa kwa mtendakazi anayejiendeleza kimasomo. Mkopo huu unalipwa moja kwa moja kwenye Chuo Husika. Riba ya mkopo huu ni 5% kwa mwaka. Mwanachama lazima awe na akiba ya kutosha kuchukua mkopo wa aina hii.

Marejesho yatakatwa moja kwa moja na mwajiri wake na kulipwa shalom saccos Limited.

MAELEZO YA UJUMLA YA MKOPO

Kwa mtendakazi yoyote anayehitaji mkopo atawasiliana na afisa mikopo au Mwenyekiti wa Mikopo kwa simu no. 0789811324 au email: asimon.tz685@gmail.com

Tarehe za kuanza kuomba mikopo ni tarehe 20/ hadi 28 ya kila mwezi na mikopo hutolewa mapema kuanzia tarehe 5-6 ya kila mwezi.

Sifa za mtu anayetakiwa kupatiwa mkopo.

1. Awe mwanachama hai ( Mwanachama hai ni mwanachama anayeweka Akiba kila mwezi au anaweza akiba kiwango cha chini cha Tshs. 240,000/= kwa mwaka)

2. Awe amekaa angalau miezi sita kwa mikopo mikubwa na angalau miezi mitatu kwa mikopo midogo au mkopo wa dharula.

3. Asiwe na deni lingine lolote lile kwenye taasisi ya fedha aliloshindwa kulipa.

4. Awe na Akiba ya kumuwezesha kupewa mkopo mara tatu ya kiasi chake cha akiba. (mkopo ni mara tatu ya akiba ya mteja).

5. Awe ana miliki hisa za Msingi 20 ambapo moja inauzwa Tshs12,300/= sawa na jumla ya Tshs.246,000/=

Karibuni watendakazi wote na Mungu atubariki katika kuwahudumia watoto wetu na Vijana vituoni.

 

About

Comments are closed.