MIKOPO YETU

Shalom saccos Limited inatoa mikopo mbali mbali kwa watendakazi wa vituo vya huduma ya mtoto na vijana Tanzania bara, lengo kubwa likiwa kuinua, kuimarisha na kuendeleza uchumi wa watumishi hao.

Watendakazi hao ili waweze kufanya kazi vizuri bila ya kuwa na vishawishi vya kujipatia fedha za haraka kupitia huduma ya mtoto na vijana; shalom saccos Limited imetengeneza mazingira salama, bora na yenye viwango vya kuvutia kuhakikisha kuwa watendakazi wote wanakuwa na fursa sawa ya kujiunga na saccos hii kwa masharti nafuu ambayo yaliandaliwa na watendakazi wenyewe.

Mikopo inayotolewa ni pamoja na mkopo wa biashara, nyumba, dharula, Elimu na kilimo na ufugaji. Aidha, mikopo hii yote inatolewa kwa dhamana ya kuwa mwanachama tu wa shalom saccos Limited.



Read More


Kikao cha wachungaji kuhusu shalom saccos Limited

Kikao cha wachungaji FPCT Singida

Kikao cha wachungaji kilichokuwa kimeandaliwa na Uongozi wa compassion International Tanzania kutoka makanisa ya washirika wenza wa kanda ya kati Dodoma wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kupata mafunzo kwa ufupi kuhusu Shalom saccos Limited. 

Wachungaji hao walifurahia sana kuona saccos hiyo jinsi inavyofanya kazi kwa umakini mkubwa na jinsi ilivyo andaa vizuri masharti ya chama(Katiba). Hata hivyo, wachungaji waliona ni vema kununua masharti ya chama hicho hata kama wao sio wanufaika wa moja kwa moja, lengo likiwa kuona jinsi watendakazi wanavyonufaika na saccos hiyo.